Spika Anne Makinda
mawasiliano yake bofya yanapatikana hapa :: +255 754 465226/+255 784 465226
amakinda@parliament.go.tz pia unaweza wasiliana naye kwa online form BOFYA HAPA
Naibu spika Ndugai mawasiliano yake bofya yanapatikana hapa
namba zake ni : +255 762 605 951 /+255 655 605 951
email: jndugai@parliament.go.tz
Tunaomba wananchi mzungumze na spika na naibu wake kwa njia ya simu hizo hapo juu ili wapete mtazamo mpana kuhusu maamuzi waliyochukua, lakini pia watanzania tuongee nao juu ya utendaji wao kwa ujumla, uvunjwaji wa Kamati ya mahesabu ya mashirika ya umma yaani POAC iwe ni sehemu ya maoni yetu kwao.
Tukiendelea kukaa kimya huku tukilalamika pembeni sio sahihi, yatupasa tuwasiliane nao ili watafakari kwa kina yale wanayoona ni maamuzi sahihi machoni pao lakini yakiwa na athari kubwa kwa taifa. Tunawasihi mtoe maoni yenye hekima na mtazamo mpana kuhusu mwenendo wa bunge kwa sasa na kamwe msitumie mwanya huu kumtukana.
Tusibaki nyuma katika kutetea mambo ya msingi katika Taifa letu, tusikae kulalamika bila kuchukua hatua yoyote hata ya kuwatumia ujumbe wa simu viongozi wetu (tumia namba hizo hapo juu), mara nyingi wanasema kwamba wanashauriwa vibaya au hizo hoja ni za kivyama, ili kuondoa visingizio hivyo sisi kama wananchi tuingilie kati na kushawishi uwepo wa POAC kama kamati muhimu kwa bunge na nchi kwa ujumla,
Tusiwape udhuru kwa kutowasiliana nao, tuwaeleze kuwa wako kwenye njia isiyo na manufaa kwa taifa. Maamuzi ya spika kufuta kamati kubwa kama POAC ni hatari kwa taifa hasa wakati huu ambao kesi na tuhuma za kufisadi taifa zinaposhamiri, lakini pia haya maamuzi ya haraka na kushitukiza yanaacha maswali magumu dhidi ya kiti cha spika? Yaani anasukumwa na nini kufanya haya mabadiliko makubwa yanayoleta udhaifu katika kusimamia mashirika yetu ya umma? Spika anafuta kamati muhimu kama hii haraka haraka na ghafla hivyo kwa sababu zipi?
Kimantiki huu ulikuwa ni wakati wa kuiongezea nguvu POAC ili kuyatolea macho vizuri (kuongeza usimamizi) haya mashirika ya umma yasiendelee na ufisadi mpya, lakini pia yamejaa uongozi mbovu. Kufutwa kwa POAC kuna manufaa kwa viongozi waandamiazi wa mashirika haya ya umma kwa misingi kwamba hawana msimamizi wa karibu. Tanzania ina uzoefu mbaya kwa mashirika ya umma yanapokosa usimamizi, ushahidi unatokana na jinsi viwanda vya nguo vilivyokufa japo kuna soko kubwa la bidhaa hiyo, shirika la ndege na vyama vya ushirika, vyote hivyo vilikufa kutokana na kukosa usimamizi bora, kwa nini tunarudi huko? Hapa tunaongea Tsh 10.5 trilioni kukosa msimamizi wa karibu!!!! Maana hiyo ndio thamani ya hayo mashirika kwa ujumla wake.
Nia yetu sio kwamba spika na naibu wake wajiudhuru ila tunataka Spika arudishe POAC.
POAC ndio jicho letu pekee kama wananchi, sisi wananchi tuna uhusiano wa moja kwa moja na wabunge kuliko hawa vigogo wanaosimamia haya mashirika, tuna nguvu zaidi dhidi wabunge wetu tuliowachagua kuliko wakurugenzi walioteuliwa. Tuna shinikizo kubwa kwa wabunge pale mambo yanapokwenda vibaya, lakini pia tuna mawasiliano mazuri na wabunge pale tunapogundua uchafu kwenye haya mashirika. Kama kukiwa na kamati inayosimamia haya mashirika ni kwamba hiyo kamati ina msaada mkubwa kutoka kwa wananchi kuhusu yanayojiri kwenye hayo mashirika, na hii itaongeza utendaji mzuri kwenye mashirika yetu ya umma. Kufuta POAC ni kuwawekea kinga vigogo wa haya mashirika ya umma, hivyo basi kama wananchi (wenye nchi) tunaomba/tunasema – (we demand as citizens) kamati ya Bunge mahesabu ya mashirika ya umma (POAC) irudishwe
Kwa nini tunataka hii kamati endelee kuwepo? Soma kazi za hii kamati (hapo chini ) jinsi zilivyo nyeti na ndio ilikuwa misingi ya kuanzishwa kwake toka awali , kama nilivyogusia hapo juu wazungu wangesema ‘’we need POAC more than ever’’ yaani tunahitaji POAC kuliko ilivyokuwa awali. Nia ni kuongeza macho kwa mafisadi wanaotamani kujinufaisha na mashirika yetu. Kwa nini leo kamati ya kusimamia mahesabu ya mashirika ya umma iogopwe hivyo? Misingi ya kuanzishwa POAC bado ipo kutokana na ukweli kwamba taifa lina mashirika yaliyo katika hali mbaya kutokana na uongozi mbovu hasa kwenye matumizi ya pesa, kwa mfano tu mashirika yafuatayo
Lakini pia tujiulize haya mamlaka ya spika kuondoa kamati yeye mtu mmoja alipewa na nani? Ina maana leo tuna nchi ambayo ina sheria au kanuni zinazovunja sheria na katiba? Yaani ni kama vile katiba imekaa kimtego kuwawezesha viongozi kufanya watakavyo?

- TANESCO
- ATC
- BANDARI
- RELI
- TAZARA
- TTCL
- Mifuko yote ya hifadhi ya jamii kuna madudu ya mikopo
- Mikabata ya madini, gasi na mafuta kuna walakini
- To scrutinize the accounts relating to existing Parastatals
- To evaluate the economic prosperity of existing Parastatal
- To scrutinize in every manner possible, the accounts, projects and other ventures of the Parastatal Corporations
- To make follow up of The Formation and Management of the Parastatal
Lakini pia tujiulize haya mamlaka ya spika kuondoa kamati yeye mtu mmoja alipewa na nani? Ina maana leo tuna nchi ambayo ina sheria au kanuni zinazovunja sheria na katiba? Yaani ni kama vile katiba imekaa kimtego kuwawezesha viongozi kufanya watakavyo?
Maoni ya Zitto Kabwe aliyekuwa mwenyekiti
Uamuzi wa Spika wa Bunge kuifuta Kamati ya POAC ni uamuzi unaorudisha nyuma juhudi za nchi kujenga asasi za uwajibikaji, ni kinyume cha sheria ya ukaguzi wa umma inayotaja Kamati tatu za Bunge za kusimamia fedha za Umma na ni kinyume cha Katiba ya nchi. Spika wa Bunge anasema kazi za Kamati ya POAC zitafanywa na Kamati ya PAC; Tanzania ina jumla ya Mashirika ya Umma 258 yenye thamani ya shilingi trilioni 10.2 mpaka mwezi Juni mwaka 2012, hata kamati ya POAC ilikuwa haiwezi kushughulikia Mashirika yote ya Umma katika mwaka mmoja, PAC itawezaje kusimamia Wizara za Serikali, Mikoa na wakala za Serikali na wakati huo huo Mashirika ya Umma 258? Kwa vyovyote vile Taifa linarudi miaka ya kabla ya 2008 ambapo Mashirika ya Umma yalikuwa kichaka cha kuiba fedha za Umma. soma zaidiKimsingi sisi kama wananchi tuna haki ya kuwasilina na spika, hakuna sheria inayozuia mwanachi kuwasiliana na kiongozi wake labda tu kiongozi husika awe ni dikiteta na anayetawala kwa mabavu tuwasiliane na spika kulinda uhai wa POAC
No comments:
Post a Comment