Sunday, August 25, 2013

MAONI NA MAPENDEKEZO KWENYE KATIBA MPYA ( #BARAZALAKATIKA #ChangeTanzania )


MAONI NA MAPENDEKEZO KWENYE KATIBA MPYA
Ø  UHURU WA KUPATA HABARI.
a)     Uhuru wa jambo hilo la kupata hapbari ni muhimu sana katika sehemu mbalimbali za nchi yetu hii ya Tanzania, hivyo tungependa kupendekeza kuwa ibara ya (30 sehemu ndogo ya 4) ni bora ifutwe katika katiba hii, kwa kuwa kuna kifungu cha 29 (2)b tayari imesha eleza juu ya umuhimu wa namna na haki ya kupata habari kama mwananchi na ni haki yake ya msingi.
b)     Tungependa kuwa ibara ya 30 (4) ni bora iwekwe kwenye sura ambazo zinahusika na usalama wa taifa sura ya 15 kwani inampa fursa na uwanja mpana wa kujadiliwa katika katiba kuliko nafasi ya kujadili ndani ya bunge kwani nafasi ya kujadili ndani ya bunge kwani nafasi yao ni ndogo  na hakuna uwanja mpana kuliko katika katiba.
c)     Kuwepo kwa vyombo vya umma ambavyo havihusiani na vyama vya siasa na view na uhuru

Thursday, August 22, 2013

Taarifa kwa umma wazungumzaji katika Baraza la Katiba la #ChangeTanzania 24/08/2013

Taarifa kuhusu Baraza la Katiba la Change Tanzania (wazungumzaji watakao kuwepo kwenye Baraza )https://www.facebook.com/events/622501621114767/ kama ilivyopangwa Tarehe 24/08/2013, 
Ili kufanikisha kutakuwa na wazungumzaji wafuatao
John Ulanga - Mkurugenzi mtendaji wa Foundation for Civil Society
Dr Azaveli Lwaitama - Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Tumaini na mhadhiri mstaafu wa UDSM
Irenei Kiria - Mkurugenzi mtendaji wa SIKIKA
Daniel Welwel - mwanasheria wa Mahakama Kuu, na mwanasheria wa Asyla Attorneys pia mwanaharakati
Deodatus Balile - Mhariri Mtendaji wa gazeti la JAMHURI

From Topics point of view:
Ulanga - Utangulizi – Tanzania tuko wapi na mwelekeo wetu kama taifa?
Dr Lwaitama na Irenei - Uwajibikaji wa taasisi na viongozi kwa wananchi na kuoanisha mfumo wa uwajibishaji
Dan Welwel - Uraia ikiwa ni pamoja na uraia mbili (dual nationality), upatikanaji wa uraia na haki za raia wa Tanzania kwa ujumla
Balile - Uhuru wa kutoa na kupata habari

Friday, August 16, 2013

#ChangeTanzania: Taarifa kwa Umma kuhusu kodi ya laini za simu ( #NoSimCardTax )


‪#‎ChangeTanzania‬ Taarifa kwa umma kuhusu KODI YA LAINI ZA SIMU ( ‪#‎NoSimCardTax‬ ) 

WITO WA WANANCHI KWA BUNGE NA SERIKALI KUHUSU TOZO/ KODI YA LAINI YA SIMU 

Hivi karibuni bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilipitisha muswada wa sheria ya fedha iliyosainiwa na rais Jakaya Kikwete na kuanza kutumika kama sheria kuanzia tarehe 01 August 2013. Sheria hii imetaja chanzo kimojawapo cha mapato kama tozo ya shilingi 1,000 kwa kila laini ya simu (sim card). 
Kama mwitikio wa sheria hii, wananchi wengi kwenye mitandao ya kijamii waliipinga tozo hii na kwa kupitia jukwaa la Change Tanzania, kuanzia tarehe 15 Julai 2013, juhudi zilianza za kukusanya maoni ya wananchi kwa njia mbili: kwa njia ya mtandao – online petition – na kwa njia ya kukusanya sahihi za wananchi mitaani.
Hadi kufikia tarehe 13 August 2013, Change Tanzania kwa njia hizi mbili imekusanya zaidi ya

Popular Posts