Mnamo tarehe 25 Juni, 2013, bajeti ya Serikali ya
mwaka wa fedha wa 2013/2014 ilipitishwa Bungeni.
Siku chache baada ya kupitishwa kwa bajeti,
ilionekana kuwa Serikali ilikuwa imeanzisha tozo ya kila mwezi ya TZS 1,000 kwa
kila kadi ya simu ya mkononi (Sim card). Jambo la kushangaza lilikuwa, wabunge
pamoja na wananchi wa kawaida waliokuwa wakifuatilia hotuba ya bajeti walidai
kuwa kodi hiyo, iliyojulikana kama “Kodi ya Kadi ya SIM”, haikujadiliwa
Bungeni. Ili lilizua mjadala wa kitaifa miongoni


