Thursday, February 19, 2015

MAMBO 20 MUHIMU YA WANANCHI YALIYOTUPWA NA KATIBA INAYOPENDEKEZWA - By @hpolepole

UNATAKA KUUJUA UKWELI BASI SOMA HAPA NA MJULISHE MWENZIO.

Katiba Inayopendekezwa ina mapungufu makubwa na imeyatupilia mbali maoni muhimu ya wananchi kama yalivyotolewa na wananchi wenyewe kama ifuatavyo;-

1. Kupunguzwa kwa madaraka ya Rais Wananchi walipendekeza madaraka makubwa ya Rais hasa ya uteuzi yapunguzwe na ziundwe Taasisi za kikatiba za kumshauri Rais kabla hajafanya teuzi. Wananchi walipendekeza pia baada ya Rais kumteua kiongozi basi itabidi mteuliwa huyo Bunge limthibitishe. Katiba Inayopendekezwa imeyafuta haya yote na imemuongezea Rais Madaraka.

2. Kutenganisha Mamlaka ya Mihimili ya Dola Wananchi walipendekeza uhuru zaidi kwa Bunge na Mamlaka zaidi kwa Bunge kuisimamia, kuiwajibisha na kuishauri Serikali. Pendekezo hili linaenda sambamba na kutenganisha serikali na Bunge, hali ambayo iko sasa. Rasimu ya Warioba ililipa Bunge Mamlaka zaidi kuisimamia Serikali na hata pale ambapo Bunge lingekataa bajeti au

Monday, December 1, 2014

Mapitio ya Change Tanzania kwa maazimio ya kamati ya PAC na maoni juu ya hatua zaidi

Change Tanzania tunatoa shukrani kwa Watanzania wote wanaoendelea kusaini tamko la kutaka uwajibikaji kamili wa serikali na bunge dhidi ya wote waliohusika katika ukwepuaji wa pesa zilizokuwa katika akaunti ya udhamini pale Benki Kuu almaarufu akaunti yaTegeta Escrow. Tunawasihi Watanzania wote wenye kutakia mema nchi yetu waendelee kusaini tamko hili https://secure.avaaz.org/en/petition/Wito_kwa_Wabunge_na_Rais_wa_Jamhuri_ya_Muungano_wa_Tanzania_WITO_WA_KUHAKIKISHA_UWAJIBIKAJI_KAMILI_UNATENDEKA_NA_PESA_ZA/share/?new .

Bila shaka sote tumeshuhudia juzi Jumamosi tarehe 29/11/2014 kamati ya PAC ikisoma tena maazimio ya bunge yaliyotokana na maridhiano baada ya mkutano wa Bunge wa ijumaa tarehe 28/11/2014 kuvunjika bila mwafaka. Change Tanzania tunapenda kutoa msimamo wetu kuhusu mapendekezo hayo yaliyotokana na mwafaka wa wabunge wa pande mbili yaani upinzani na chama tawala CCM. Tunawapongeza wabunge kwa kupiga hatua kukubaliana juu ya hatua za mwanzo kuelekea uwajibikaji wa viongozi na wahusika katika ukwepuaji wa fedha hizi za umma. Hata hivyo mojawapo ya matakwa ya tamko letu wananchi ilikuwa ni uwajibikaji kamili wa wahusika serikalini. Kutokana na ripoti ya PAC iliyojengwa juu ya ripoti maalum ya ukaguzi wa CAG na ushahidi wa PCCB uhusika wa viongozi wa serikali ni mpana sana katika jambo hili na unatambuka katika wizara zaidi ya moja, ni wazi kuwa Kiongozi wa shughuli za kila siku wa serikali ambaye kwa mujibu wa

Saturday, September 14, 2013

UTAFITI WA @Twaweza_NiSisi : 83% ya watu hawaikubali kodi ya sh 1,000 kwa mwezi kwa kila laini ya simu #NoSimCardTax

FOR ENGLISH SEE BELOW
 Mnamo tarehe 25 Juni, 2013, bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha wa 2013/2014 ilipitishwa Bungeni.

Siku chache baada ya kupitishwa kwa bajeti, ilionekana kuwa Serikali ilikuwa imeanzisha tozo ya kila mwezi ya TZS 1,000 kwa kila kadi ya simu ya mkononi (Sim card). Jambo la kushangaza lilikuwa, wabunge pamoja na wananchi wa kawaida waliokuwa wakifuatilia hotuba ya bajeti walidai kuwa kodi hiyo, iliyojulikana kama “Kodi ya Kadi ya SIM”, haikujadiliwa Bungeni. Ili lilizua mjadala wa kitaifa miongoni

Sunday, August 25, 2013

MAONI NA MAPENDEKEZO KWENYE KATIBA MPYA ( #BARAZALAKATIKA #ChangeTanzania )


MAONI NA MAPENDEKEZO KWENYE KATIBA MPYA
Ø  UHURU WA KUPATA HABARI.
a)     Uhuru wa jambo hilo la kupata hapbari ni muhimu sana katika sehemu mbalimbali za nchi yetu hii ya Tanzania, hivyo tungependa kupendekeza kuwa ibara ya (30 sehemu ndogo ya 4) ni bora ifutwe katika katiba hii, kwa kuwa kuna kifungu cha 29 (2)b tayari imesha eleza juu ya umuhimu wa namna na haki ya kupata habari kama mwananchi na ni haki yake ya msingi.
b)     Tungependa kuwa ibara ya 30 (4) ni bora iwekwe kwenye sura ambazo zinahusika na usalama wa taifa sura ya 15 kwani inampa fursa na uwanja mpana wa kujadiliwa katika katiba kuliko nafasi ya kujadili ndani ya bunge kwani nafasi ya kujadili ndani ya bunge kwani nafasi yao ni ndogo  na hakuna uwanja mpana kuliko katika katiba.
c)     Kuwepo kwa vyombo vya umma ambavyo havihusiani na vyama vya siasa na view na uhuru

Thursday, August 22, 2013

Taarifa kwa umma wazungumzaji katika Baraza la Katiba la #ChangeTanzania 24/08/2013

Taarifa kuhusu Baraza la Katiba la Change Tanzania (wazungumzaji watakao kuwepo kwenye Baraza )https://www.facebook.com/events/622501621114767/ kama ilivyopangwa Tarehe 24/08/2013, 
Ili kufanikisha kutakuwa na wazungumzaji wafuatao
John Ulanga - Mkurugenzi mtendaji wa Foundation for Civil Society
Dr Azaveli Lwaitama - Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Tumaini na mhadhiri mstaafu wa UDSM
Irenei Kiria - Mkurugenzi mtendaji wa SIKIKA
Daniel Welwel - mwanasheria wa Mahakama Kuu, na mwanasheria wa Asyla Attorneys pia mwanaharakati
Deodatus Balile - Mhariri Mtendaji wa gazeti la JAMHURI

From Topics point of view:
Ulanga - Utangulizi – Tanzania tuko wapi na mwelekeo wetu kama taifa?
Dr Lwaitama na Irenei - Uwajibikaji wa taasisi na viongozi kwa wananchi na kuoanisha mfumo wa uwajibishaji
Dan Welwel - Uraia ikiwa ni pamoja na uraia mbili (dual nationality), upatikanaji wa uraia na haki za raia wa Tanzania kwa ujumla
Balile - Uhuru wa kutoa na kupata habari

Friday, August 16, 2013

#ChangeTanzania: Taarifa kwa Umma kuhusu kodi ya laini za simu ( #NoSimCardTax )


‪#‎ChangeTanzania‬ Taarifa kwa umma kuhusu KODI YA LAINI ZA SIMU ( ‪#‎NoSimCardTax‬ ) 

WITO WA WANANCHI KWA BUNGE NA SERIKALI KUHUSU TOZO/ KODI YA LAINI YA SIMU 

Hivi karibuni bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilipitisha muswada wa sheria ya fedha iliyosainiwa na rais Jakaya Kikwete na kuanza kutumika kama sheria kuanzia tarehe 01 August 2013. Sheria hii imetaja chanzo kimojawapo cha mapato kama tozo ya shilingi 1,000 kwa kila laini ya simu (sim card). 
Kama mwitikio wa sheria hii, wananchi wengi kwenye mitandao ya kijamii waliipinga tozo hii na kwa kupitia jukwaa la Change Tanzania, kuanzia tarehe 15 Julai 2013, juhudi zilianza za kukusanya maoni ya wananchi kwa njia mbili: kwa njia ya mtandao – online petition – na kwa njia ya kukusanya sahihi za wananchi mitaani.
Hadi kufikia tarehe 13 August 2013, Change Tanzania kwa njia hizi mbili imekusanya zaidi ya

Monday, July 15, 2013

WITO WA KUSITISHA TOZO/KODI YA LAINI YA SIMU KUFUATIA MABADILIKO YA SHERIA YA KODI 2013


CHANGE TANZANIA timu! Wakati ni kwetu kuonyesha kuwa mabadiliko ni sisi na si kusubiri mtu mwingine alete mabadiliko. Tembelea tovuti hii (http://www.avaaz.org/en/petition/WITO_WA_KUSITISHA_TOZOKODI_YA_LAINI_YA_SIMU_KILA_MWEZI_KUFUATIA_MABADILIKO_YA_SHERIA_YA_KODI_2013/?copy  na uweke sahihi yako kupitia mtandao ili kuikataa kodi au tozo kandamizi ya  laini ya  simu (Sim card tax). Tusaidiane tukusanye sahihi milioni moja ili tuweze kuiwasilisha bungeni mwezi wa nane . Ni dakika chache tu toa muda wako muhimu kulijenga Taifa lako, watanzania tumekuwa na utamaduni wa muda mrefu wa kulalamikia vitu na kuvihacha viendelee japo atukubaliani navyo, kwa kusaini hapo kwenye link kwa pamoja tutakuwa na sauti moja katika ili, pia itasaidia kumtetea mwananchi wa hali ya chini ambaye ndo anaumizwa sana  na kodi au tozo hii kandamizi kila mwezi, serikali inaweza bana matumizi ili kutekeleza bajeti yake, pia kuna vyanzo vingine vya kodi kama tulivyoelezea kwenye hiyo petition. Shawishi na wenzako angalau 100 waweze saini zao pia, kwa kadri tunakavyoweza pata idadi kubwa ndivyo tutakavyopata uwezo wa kusimamisha hii kodi, nchi ni wananchi, sisi ni wananchi.
   Mabadiliko kwa vitendo.

Sunday, June 16, 2013

Maoni ya mdau wa changetanzania juu ya bajeti 2013/2014

1. UTANGULIZI.

Haya ni maoni yangu kuhusu Bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha 2013/2014. Nimeisoma bajeti yote, hivyo mchango wangu nimeuweka kwenye vipengele vikuu vitatu:

1.) Mipango Mizuri - kwa ajili ya kuwapa motisha viongozi na kuboresha zaidi,

2.) Mipango ya Kurekebisha - ambayo naona ni kandamizi kwa mwananchi, na

3.) Mtazamo wa Jumla na Mapendekezo.

Kwa mambo ambayo nimeona ni ya kawaida sitayagusia; lakini jambo ambalo kwangu ni la kawaida ila kwa wananchi wenzangu linaweza kuwa la mashaka kwao limeligusia.Soma kwa undani hapa changetanzania official website 

Thursday, May 16, 2013

Habari Muhimu kuhusu #Tanzania

1.)  Tanzania: BVR Is for Voter Registration, Not Voting, Says NEC
IN a bid to improve transparency, the National Electoral Commission (NEC) plans to introduce biometric voter registration (BVR) to replace the existing Permanent National Voters Register (PNVR) ahead of the general elections in 2015. Read more 

PRESIDENT Jakaya Kikwete has appointed Ambassador Liberata Mulamula to be Tanzanian Ambassador to the US in Washington.
Prior to the appointment, Ambassador Mulamula was the Senior Diplomacy Advisor to the President. She previously served as the Executive Secretary of the Secretariat of the International Conference of the Great Lake Region (ICGLR) for four years (Januray 2007-December 2010) Read more

3.) Tanzania: 'Cut Down On Tax Exemptions 
AS the Tanzania Revenue Authority (TRA) targets to boost revenue collections to about 18tri/- annually in five years time, Denmark has expressed the need to cut down on tax exemptions to boost revenue collection.
The recent Controller and Auditor General (CAG) report revealed that tax exemptions has reached 1.8tri/-, which is almost 4.6 times of the 8.3tri/-projected to be collected in this financial year Read More

kwa hisani ya  allafrica.com

Friday, March 15, 2013

Mkuu wa wilaya KOROGW E :Changamoto za elimuyetu hapa korogwe

Mkuu wa wilaya KOROGWE, TANGA  ndugu Mrisho Gambo amekutana na haya katika idara ya elimu huko Korogwe baada ya kufanya uchunguzi mdogo wa nini kinaendelea hasa katika matumizi ya pesa, halichokutana nacho ni hiki:
            TAARIFA FUPI


Naendelea kufanyia kazi changamoto za Elimu yetu hapa Korogwe.
Jana nilikutana na Idara za Elimu Sekondari kupitia matumizi ya pesa za kununua vitabu na

MAHITAJI YA NG’OMBE ILI AONGEZE MAZIWA


Wape ng’ombe wako lishe kamili, yenye nguvu, protini, na vitamin pamoja na maji ya kutosha. Kulisha ng’ombe kwa kutumia aina yoyote ya malisho haitoshi kukuhakikishia ng’ombe anakuwa na afya nzuri na kutoa maziwa ya kutosha. Kama ilivyo kwa binadamu, ng’ombe anahitaji mlo kamili. Malisho ni lazima yawe na uwiano sahihi wa viungo.
Mifugo inahitaji chakula kitakachowapa nguvu, protini, madini, na vitamin ili kujenga miili yao, kuzalisha maziwa, na kuzaliana. Wanyama wadogo wanahitaji virutubisho vya kutosha, ili wakuwe na kuongeza uzito. Ng’ombe wa maziwa wanahitaji virutubisho zaidi ili kuweza kuzalisha maziwa kwa wingi hasa katika kipindi cha miezi 3-4 ya mwanzo baada ya kuzaa, wakati ambao uzalishaji wa maziwa unakuwa juu.

Malisho ya kijani ni mlo mkuu kwa mifugo
Mlo muhimu na wenye virutubisho kwa mifugo ni majani. Lakini soma zaidi

Wednesday, March 13, 2013

DEDICATED EFFORTS WILL STOP ACUTE KIDNEY ATTACKS


As kidney disease threaten many life in the world i have honour to share to you a World Kidney Day (WKD), It is a global health awareness campaign focusing on the importance of the kidneys and reducing the frequency and impact of kidney disease and its associated health problems worldwide. The campaign is celebrated every year on the second Thursday of March in more than 100 countries on 6 continents. READ MORE

Tuesday, March 5, 2013

NAFASI YA WALIMU WAPEWE WALIMU NA WATHAMINIWE


Tukubali tukiamini walimu wanajua matatizo yanayoikumba Elimu kuliko mtu mwingine yeyote. Tuwapatie fursa stahiki katika kuleta suluhu matatizo ya Elimu nchini.
Mwalimu ni mlezi wa kiroho, kiakili na kimwili wa wanafunzi. Tatizo la ufaulu mdogo wa wanafunzi wahitimu wa kidato cha 4 mtihani wa mwaka 2012 kwa sehemu kubwa na kwa kiasi kikubwa ni matokeo ya malezi duni, kiroho, kimwili na kiakili ambapo mwalimu amenyang'anywa jukumu lake na kuachiwa kisehemu kidogo tu katika malezi ya kiakili kwa kuwafundisha watoto majibu ya SOMA ZAIDI 

Popular Posts