Change Tanzania tunatoa shukrani kwa Watanzania wote wanaoendelea kusaini tamko la kutaka uwajibikaji kamili wa serikali na bunge dhidi ya wote waliohusika katika ukwepuaji wa pesa zilizokuwa katika akaunti ya udhamini pale Benki Kuu almaarufu akaunti yaTegeta Escrow. Tunawasihi Watanzania wote wenye kutakia mema nchi yetu waendelee kusaini tamko hili https://secure.avaaz.org/en/petition/Wito_kwa_Wabunge_na_Rais_wa_Jamhuri_ya_Muungano_wa_Tanzania_WITO_WA_KUHAKIKISHA_UWAJIBIKAJI_KAMILI_UNATENDEKA_NA_PESA_ZA/share/?new .
Bila shaka sote tumeshuhudia juzi Jumamosi tarehe 29/11/2014 kamati ya PAC ikisoma tena maazimio ya bunge yaliyotokana na maridhiano baada ya mkutano wa Bunge wa ijumaa tarehe 28/11/2014 kuvunjika bila mwafaka. Change Tanzania tunapenda kutoa msimamo wetu kuhusu mapendekezo hayo yaliyotokana na mwafaka wa wabunge wa pande mbili yaani upinzani na chama tawala CCM. Tunawapongeza wabunge kwa kupiga hatua kukubaliana juu ya hatua za mwanzo kuelekea uwajibikaji wa viongozi na wahusika katika ukwepuaji wa fedha hizi za umma. Hata hivyo mojawapo ya matakwa ya tamko letu wananchi ilikuwa ni uwajibikaji kamili wa wahusika serikalini. Kutokana na ripoti ya PAC iliyojengwa juu ya ripoti maalum ya ukaguzi wa CAG na ushahidi wa PCCB uhusika wa viongozi wa serikali ni mpana sana katika jambo hili na unatambuka katika wizara zaidi ya moja, ni wazi kuwa Kiongozi wa shughuli za kila siku wa serikali ambaye kwa mujibu wa