Monday, June 18, 2012
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA, BAJETI 2012/2013
Ili kuweka kumbukumbu sawa hii hapa chini ni hotuba
Labels:
Uchumi
Sunday, June 3, 2012
Hotuba Ya Raisi Kikwete
Kama ilivyo ada, namshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehma, kwa kutujaalia uhai na kutuwezesha kumaliza mwezi Mei salama. Kwa kutumia utaratibu wetu wa kuzungumza kwa njia hii kila mwisho wa mwezi, leo nitazungumzia mambo matatu.
Mkutano wa G-8Jambo la kwanza, ni suala la usalama wa chakula na lishe. Duniani, inakadiriwa kuwa kuna watu milioni 925 wanaokabiliwa na njaa na lishe duni. Kati ya hao Afrika ina watu milioni 239 ambao ni karibu theluthi moja ya watu wote wenye tatizo la njaa na lishe duni kote duniani.
Nchi za Afrika zenye tatizo la njaa kiasi cha kuhitaji msaada wa chakula kutoka nje ni 27. Kati ya hizo 11 zina matatizo makubwa zaidi. Tanzania siyo miongoni mwa nchi hizo, hata hivyo bado hatujafikia kiwango cha kujitosheleza kabisa. Hivi sasa tumefikia asilimia 95 na kila mwaka yapo maeneo nchini yanayopata msaada wa chakula kutoka Serikalini.
Mwaka 2009, katika mkutano wao wa L’Aquila, Italia, viongozi wa nchi nane tajiri kuliko zote duniani waliamua kuchukua hatua ya kuzisaidia nchi zinazoendelea duniani kukabiliana na tatizo la njaa na lishe duni. Katika mkutano ule waliahidi kutoa dola za Marekani bilioni 22 kwa ajili hiyo. Tanzania tunategemea kupata
Subscribe to:
Posts (Atom)
