Jana (sio jana) nilipata challange kutoka kwa dada maria kuhusu kutengeneza
baraza la mawaziri lenye wizara 10-15 baraza dongo lakini hatukuafikia
pale nilipo mwambia ningependa kuwe na manaibu waziri kwenye baadhi ya
wizara.Katika mjadala wangu na dada maria twitter nilionyesha wizara zangu 10
+ wizara ndogo 3 hapa ukimweka na waziri mkuu unapata baraza la
mawaziri lenye mawaziri kamaili 14.
Lakini nikajenga hoja kutakuwa na wizara kama 7 ambazo
kutakuwa na ma
naibu waziri.
Kivipi Mfano wizara ya Fedha na Uchumi ni wizara kubwa hivyo
ningependa pawe na msadizi naibu waziri kuweza kumsaidia waziri wa
fedha kwenye shughuli mbalimbali.
Lakini pia kuna wizara kama ya Miundombinu na Uchukuzi wizara hii ni
kubwa Miundombinu inabeba barabara zetu zote ujenzi wake na kila.pia
kuna uchukuzi ndani ya usafirishaji nao ni mpana kuna
ndege,maji,barabara lazma wapate naibu waziri ili mzigo usiwe mkubwa
kwa waziri.
Mchanganuo wangu wa wizara ulikua kama ufatavyo
Waziri mkuu
1.Nishati na Madini
2.Uchumi na Fedha
3.Miundombinu na uchukuzi
4.Kilimo,Maji Na Ardhi
5.Vijana na Maendeleo ya Jamii(Wanawake)
6.Viwanda Biashara na Uwekezaji
7.Mambo ya Nje na Africa Mashariki + Muungano
8.Mambo ya Ndani
9.Jeshi Na Technology
10.Ajira
Wizara 3 ndogo
1.Michezo na utamaduni
2.Ufisadi Rushwa Uwajibikaji na Madili Bora
3.Uchunguzi(Research)
Sasa hizo ndo wizara zangu kwa maono yangu hapa mawaziri wote
hawatakuwa wabunge kusiwe na double standard kwenye maamuzi.
Pia watu watajiuliza kwanini Jeshi nimeka na technology nimefanya
hivyo ili jeshi lilinde technology yetu lifanye ugunduzi wa new
technology.
Kwanini kuna wizara ndogo ya research hii wizara itajitahidi kugundua
vitu vipya na kufanya ugunduzi ni kipya hapa tanzania.
Kama tunavyoona ni baraza dongo lenye kupitia kila kitu na kubana matumizi tu.
Kwa taarifa hili baraza litaendeshwa na serikali ya majimbo yenye
ufanisi zaidi vyeo kama vya ukuu wa wilaya na mkoa vitakufa kutakua na
Mkuu wa jimbo la kusini.
Hii itasaidia kwenye maendeleo ya haraka katika nchii yetu baraza ni
dogo sana lenye ufanisi na mambo mapya hapa nchini tanzania.
Kumbukumbu tu:
Mimi ni mtu wa kawaida kijana,kapuku tu kama wengine mwenye kutaka mabadiliko
By Fred Kavishe
No comments:
Post a Comment