Tuesday, May 29, 2012

Migongano baina ya wazanzibari na watanganyika haikuanza baada ya muungano mwaka 1964

Makala ya Mdau
Interraction baina ya wazanzibari na watanganyika haikuanza baada ya muungano mwaka 1964. Kwa mujibu ya wazee waliotutangulia, wanadai, hapo kale walikuwa wakivuka kwa majahazi kuja kufanya biashara Tanganyika na wafanyakazi wengi wa kule visiwani hasa Pemba walikuwa wanatoka Bara, walijulikana kwa jina la pamoja kuwa WANYAMWEZI.

Mzee aliyenipa simulizi hizi anadai yeye alikuja bara kabla ya muungano lakini si peke yake bali hata huyo Karume walikuwa nae Tanganyika kabla hata ya mapinduzi ya zanzibar. Wapo watanganyika na wazanzibar waliooana kabla ya muungano na wapo waliohamisha makazi yao kuelekea bara au visiwani kabla ya ya muungano na analaani UROHO WA KISIASA wa wanasiasa wa Zanzibar na Tanganyika wa kipindi hicho kwa kutumia undugu na muingiliano baina ya bara na visiwani on their political advantage.
Karume kwa upande wake alikuwa na sababu zake binafsi za kuingia kwenye muungano na Nyerere pia alikuwa na sababu zake binafsi ambazo, kwa namna moja au nyengine zimechangia kuufanya muungano huu
wa kisiasa kulega lega.

“unajua karume alitiwa upofu na matatizo yake yaliyokuwa yanamkabili kwa wakati ule hivyo, terms zozote
za muungano zilikuwa zinamfaa yeye binafsi, na Nyerere hivyo hivyo” nilimnukuu mzee huyo

DHANA YA KUWA KARUME NDIYE ALIYETAKA MUUNGANO:

Karume hakuwa mtu mwenye mvuto wa kisiasa, hata malezi yake na ukuwaji wake hauna asili ya zanzibar, wapo wanaosema Karume ni MNYASA, na wapo baadhi ya wazee wanadai karume aliondoka Zanzibar akiwa na umri mdogo kuelekea Tanganyika na baadae Uingereza kisha akarudi Tanganyika ambapo alikua
kiongozi wa chama cha mabaharia.

Wapo wanaoamini karume aliwekwa tu Urais wa zanzibar baada ya mapinduzi lakini wapo wanaoamini Karume alishiriki kikamilifu katika mapinduzi. Jambo moja linalojulikana kwa usahihi kabisa ni kwamba usiku wa mapinduzi, Karume alikuwa Tanganyika katika shughuli zake za kila siku na alirudi Zanzibar akasimikwa kuwa Rais
Watu waliokuwa na mvuto mkubwa wa kisiasa pale visiwani akina abdulrahman BABU, Othman shariff, Abdallah kassim Hanga na kina Twala, ambao kwa kiasi kikubwa walifanikisha mapinduzi ya zanzibar walikuwa tishio kubwa kwa Bwana Karume. Kwanza alianza kwa kupiga marufuku chama chao cha UMMA PARTY hivyo kuwaleta karibu maadui zake kwenye ASP, KARUME akabaki na option moja tu, kuomba usaidizi wa Tanganyika.

“Unajua akina babu na othman shariff walikuwa na nguvu kuliko karume hivyo mzee karume akaamua
aungane na tanganyika ili moja awape mamlaka maadui zake kwenye serikali ya muungano ili ajipunguzie tishio la kupinduliwa lakini pili asingeweza washughulikia akiwa peke yake” aliendelea mzee huyo
So kwa upande wa karume muungano ulikuwa kwa ajili ya kujilinda yeye dhidi ya kupinduliwa na kwamba alitaka muungano wa muda mfupi atimize malengo yake na huko mbele tutaelezea jinsi karume alivyowahukumu na kuwaua wale wote waliosemekana ni maadui zake wa kisiasa na ambao pia walikuwa mashahidi wa utiaji saini wa mkataba wa muungano.
lakini kwa upande wa nyerere, mwaka 1963 na 64 ndio kilikua kipindi chake kigumu katika utawala na alinusurika majaribio machache cha kutaka kupinduliwa, kwa upande wa pili Zanzibar ilikuwa inakuwa kwa kasi na kwamba kumiliki visiwa hivyo viwili ingeongeza ulinzi wa bara na pili kupunguza tishio la kupinduliwa.

SHINIKIZO TOKA MAGHARIBI
Sababu hii, na ile ya karume dhidi ya BABU na wenzie ndizo zenye uzito mkubwa. Soon after Revolution Zanzibar ilijitangaza kuwa taifa la kikomunist na kuwafukuza visiwani raia wa Uingereza huku ikiimarisha uhusiano wake na CUBA, RUSSIA na CHINA.
Zanzibar pia ilikuwa nchi ya kwanza Africa kuitambua serikali ya EAST GERMAN na Baadae NORTH KOREA uthibitisho tosha kuwa ilikuwa kinara wa ukomunist afrika..
Che guevara katika kitabu chake page ya 348 anaandika kuwa “Zanzibar is our friend and we gave them our small bit of assistance, our fraternal assistance, our revolutionary assistance at the moment when it was necessary..
Kwa wakati ule, Zanzibar ilikuwa ikijulikana kama havana of Afica huku abdulrahman Babu na wenzie akina Othman shariff wakiwa vinara wa ukomunist africa.
Katika simulizi za huyu mzee anadai Babu na vijana 22 kati ya mwaka 1958 na 1963 walienda cuba na venezuela kupata mafunzo ya mapinduzi chini ya ernesto che guevara jinsi ya kufanya mapinduzi na vijana hao (umma cadres) ndio walioshika sehemu muhimu kama palace na kituo cha tv wakati wa mapinduzi.
Unajua zanzibar ilikuwa kitovu cha ukomunist Afrika, kumbuka hata baada ya mapinduzi ya zanzibar, nchi za kikomunist ndio zilikuwa za kwanza kutambua serikali ya mapinduzi hivyo ikawalazimu waingereza na wamarekani kumshawishi nyerere ambaye wakati ule wa mwaka 64 alikuwa anategenea msaada wa waingereza kumlinda dhidi la vuguvugu la mapinduzi na hivyo nyerere hakuwa na option.

Ikumbukwe pia mambo haya ya ukomunist wa zanzibar yalikuwa yanatokea at the heart of cold war, anihadithia mzee huyu kama meli za kivita za uingereza akikumbuka majina kama HMS owen, royal fleet auxilliary HEBE na FRIGATE RHYL zilikuwa zikivinjari katika pwani ya zanzibar tayari kwa jambo lolote.

Kutokana na maelezo ya wazee mbalimbali walioishi zanzibar wakati wa muungano, wanaamini zanzibar iliungana na tanganyika kwa shinikizo la nchi za magharibi kwa upande mmoja lakini pili, kwa maombi ya karume ili apate ulinzi dhidi ya adui zake ambao walikuwa na umaarufu kisiasa pale visiwani kuliko yeye.

KATIKA MAKALA IJAYO, TUTALETA USHAHIDI WA KUELEZA KILE KINACHOAMINIKA KUWA MUUNGANO ULIKUWA NI WA MIAKA 10 TU YAANI 1964-74 NDANI YAKE TUTAELEZA NINI KILIWAKUTA WALIOKUWA MAADUI WA KARUME AMBAO NDIO SIGNATORY WA MKATABA WA MUUNGANO NA MWISHO KIFO CHA KARUME MIAKA 2 KABLA YA MWAKA WA KUVUNJIKA KWA MUUNGANO

1 comment:

  1. What a nice presentation! keep on sharing the knowledge.Thanks author

    ReplyDelete

Popular Posts