MAONI NA MAPENDEKEZO KWENYE KATIBA
MPYA
Ø
UHURU WA
KUPATA HABARI.
a) Uhuru
wa jambo hilo la kupata hapbari ni muhimu sana katika sehemu mbalimbali za nchi
yetu hii ya Tanzania, hivyo tungependa kupendekeza kuwa ibara ya (30 sehemu
ndogo ya 4) ni bora ifutwe katika katiba hii, kwa kuwa kuna kifungu cha 29 (2)b
tayari imesha eleza juu ya umuhimu wa namna na haki ya kupata habari kama
mwananchi na ni haki yake ya msingi.
b) Tungependa
kuwa ibara ya 30 (4) ni bora iwekwe kwenye sura ambazo zinahusika na usalama wa
taifa sura ya 15 kwani inampa fursa na uwanja mpana wa kujadiliwa katika katiba
kuliko nafasi ya kujadili ndani ya bunge kwani nafasi ya kujadili ndani ya
bunge kwani nafasi yao ni ndogo na
hakuna uwanja mpana kuliko katika katiba.
c) Kuwepo
kwa vyombo vya umma ambavyo havihusiani na vyama vya siasa na view na uhuru
wa
kutoa habari pasipo kuwa na vikwazo katika katiba za vyama mbalimbali vya
siasa.
d) Pia
serikali isiingilie uhuru wa habari kwa
upande wa bajeti ya vyombo hivyo, tunapendekeza kuwa ni bora bunge liwajibike katika usimamizi wa
bajeti zao.
e) Mwisho
katika hili la habari, tunaomba kuwe na tume huru ya usajili na usimamizi wa
vyombo vya habari, ambayo ipendekezwe na uteuzi ufanywe ndani ya bunge.
Ø
UWAJIBIKAJI
WA TAASISI NA VIONGOZI KWA WANANCHI NA KUOANISHA MFUMO WA UWAJIBIKAJI.
a) Haki
ya ajira kwa vijana katika taratibu za ujira au katika katiba hii mpya ambayo
haijafafanua rasmi hujira kwa vijana kwani ajira zinazo tolewa kwa vijana
zimewabana sana vijana ususani wanao toka vyuoni yaani wahitimu kwa kutakiwa
kuwa na uzoefu wa zaidi ya miaka 2, kwa hiyo kuna wataka vijana kuwa na uzoefu
ni vyema wawaandalie, serikali iwagharamie vijana kwa kuwapa ruzuku ili wapate
uzoefu.
b) Haki
ya wajane: katika rasimu hii haijaonyesha haki za wajane kama haki zingine kwa
hiyo kwenye katiba hii tunapendekeza kuwe na haki ya wajane.
c) Katiba
hii haijafafanua huduma ya watu maalum kama vile walemavu, kwa kupata elimu
bora, ulinzi, malazi na tiba.
d) Katiba
hii inasema Ardhi ni mali ya raisi kwa hiyo tunaomba Ardhi iwe mali ya mwananchi
isipokuwa serikali iweke utaratibu mzuri kwa wananchi waweze kugawana Ardhi
vizuri kama mali yao.
e) Haki
ya elimu, rasimu hii ya katiba inasema kila mtu anahaki ya kupata elimu bora,
lakini tunaona bado kuna ukandamizaji wa elimu kwa kufuata wenye kipato na kuwabaguwa
wasio na kipato kama vile shule binafsi wanasoma watoto wa matajiri tu, kwa
hiyo tunaomba rasimu rasimu hii ifafanue kipengele hicho upya.
f) Haki
ya waliopata ajali, katika rasimu hii haikuongelea kabisa haki ya waliopata
ajali na kuwa vilema, hivyo tunapendekeza kuwa wahudumiwe na serikali kwa
kuwapa mahitaji mbalimbali.
g) Uhuru
wa ndoa katika jamii, katika rasimu hii ya katiba, kulingana na sheria ya ndoa
ya mwaka 1971na kufanyiwa marekebisho mwaka 2002 inaweka wazi uhuru wa ndoa, na
kwa kutokuwa na mwingiliano kwa wazazi na wanandoa pamoja na koo kwa koo au
kabila kwa kabila. Kwa hiyo tunapendekeza kuwa katika katiba ijayo iweke vizuri
sheria ya ndoa kwenye katiba mpya.
h) Ibara ya 92(4) Neno "Hazitakuwa" ifutwe
na Neno "Vitakuwa" liwekwe badala yake
i) Ibara ya 96(3)
Mawaziri wawajibike mmoja mmoja bungeni
j) Ibara ya 115(2)
kirekebishwe na endapo Bunge litakataa kwa Mara ya pili kwa kura zaidi ya
theluthi mbili basi Rais atalazimika kuvunja Baraza la Mawaziri
k) Ibara ya 108(2)
kifutwe kwa sababu kinapoka mamlaka ya Bunge ya Kuisimamia na Kuiwajibisha
Serikali.
l) Ibara ya 113(1)
ifutwe kwa sababu inapoka Mamlaka ya Bunge kama yalivyoainishwa kwenye Ibara ya
107(1)
m) Ibara 200(1)
Uteuzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ufanywe na Bunge baada
ya kupendekezwa na tume ya utimishi ya Bunge.
n) Ibara ya 202(4)
Kirekebishwe.Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali awasilishe ripoti
ya Ukaguzi Bungeni badala ya Rais.Atakapowasilisha Bunge lijadili hiyo ripoti
na kutoa mapendekezo na inapohitajika hatua stahiki
o) Ibara ya 202(5)
kifutwe.
p) Ibara ya 204(5)
Mamlaka ya kumwondoa kazini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali yawe
ya Bunge na si Rais.Hii ni kuimarisha dhana ya Uwajibikaji.
q) Rasimu iko
kimya kuhusu utaratibu wa kumwondoa Jaji Mkuu kazini.Utaratibu wa kumwondoa
Jaji Mkuu madarakani uwe sawa sawa na ule unaotumika katika kumwondoa Rais
madarakani.Hii itakazia Uhuru wa mhimili wa Mahakama katika kufanya shughuli
zake.
r) Bajeti ya
Mahakama ikipitishwa na Bunge basi itolewe bila kucheleweshwa au
kubadilishwa.Iwe marufuku kwa hazina kubadilisha matumizi ya bajeti ya Mahakama
kwa namna yeyote ile.
Ø
URAIA IKIWA NI PAMOJA NA URAIA
MBILI, UPATIKANAJI WA URAIA NA HAKI ZA RAIA WA TANZANIA KWA UJUMLA.
a) Katika ibara ya 37 (2) hakuna
mamlaka yeyote wala sheria itayotungwa na bunge la jamhuri ya muungano wa
Tanzania itakayomuondolea mwanachi uraia wake wa kuzaliwa kwa lazima.
b) Kila raia ana haki ya
kutambuliwa uraia wakekwa madhumuni hayo bunge liunde sheria, itungwe sheria
hii ilikuweka masharti pindi madhara kama haya yakitokea baada ya utaratibu
utaowekwa kisheria kufatwa.
c) Katiba ijayo iweke wazi kuhusu Uraia
uwe wa chi moja tu, uraia ni haki ya binaadamu kila mtu ana haki ya kuishi na kupata mahitaji yote
muhimu kama raia katika nchi yake.
d) Ibara ya 1 (2) neon Tanzania
bara litolewe iandikwe kuwa ni jamhuri ya Tanganyika.
.
No comments:
Post a Comment