Mkuu wa wilaya KOROGWE, TANGA ndugu Mrisho Gambo amekutana na haya katika idara ya elimu huko Korogwe baada ya kufanya uchunguzi mdogo wa nini kinaendelea hasa katika matumizi ya pesa, halichokutana nacho ni hiki:
TAARIFA FUPI
Naendelea
kufanyia kazi changamoto za Elimu yetu hapa Korogwe.
Jana
nilikutana na Idara za Elimu Sekondari kupitia matumizi ya pesa za kununua
vitabu na
vifaa vya kufundishia pamoja na maabara mashuleni.
Nilisema
nisianzie mbali sana, nianze toka 2010! Maana bila vitabu na vifaa vya
kufundishia hatuwezi kupata Elimu bora.
Jana
niliona maajabu na vituko, kwenye baadhi ya shule za sekondari yamekwenda
mamilion lakini hakuna vitabu vilivyo nunuliwa. Hata hizo taarifa zilizo
andikwa inawezekana zikawa ni za kwenye makaratasi tu na power point.
Ukiuliza
unaambiwa mkuu wa shule hapa alipata uchizi, pale alifariki ndo maana hakuna
taarifa. Huu ni utani!
Nilihoji
Mbona shule hazina maabara lakini pesa za maabara zimetumika? Kwanini Bodi za
shule hazishirikishwi? Kwanini walimu hawashirikishwi? Kwanini taarifa za pesa
hizi haziendi kwenye mabaraza ya kata? Kwanini taarifa hizi hazitolewi kwenye
mikutano mikuu ya vijiji?
Maana
hizi ni pesa za umma! Haziitaji usiri wowote.
Sasa
nimeamua Mimi na kamati yangu ya Ulinzi na Usalama kupita shule moja baada ya
nyingine kukagua vitabu physically.
Tusubiri
matokeo, nataka kuwa TOMASO!
Mrisho Gambo
Mrisho Gambo
No comments:
Post a Comment